Balaza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita limewafuta kazi watumishi 3 wa Halmashauri hiyo kwa Mujibu wa Kanuni za Kiutumishi .
Akitoa Taarifa hiyo katika kikao Maalumu kilichoketi mara Baada ya kukamilika kwa Balaza la Madiwani Mwenyekiti wa Balaza hilo Ambaye pia ni Diwani wa kata ya Butobela Charles Kazungu amesema watumishi hao wamefutwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya Utoro kazini.
“Balaza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa Kauri Moja limekwenda kuwafuta kazi au kuwasimamisha kazi kuwafuta kazi watumishi watatu kwasababu ya kanuni zetu za kiutumishi ,” Mwenyekiti wa Balaza la Madiwani Kazungu.
Kazungu amewataja watumishi hao kuwa ni Aden Benard ambaye ni Afisa Mtendaji katika Kijiji cha Nzera, John Misango Afisa Mtendaji Kijiji, na Walter Innocent ambaye pia alikuwa ni Mteknolojia Maabala pia Balaza linaendelea kuwachungunza watumishi wawili akiwemo Mussa Alfredy ambaye ni Afisa Tabibu Msaidizi pamoja na Elisha Makaja ambaye pia ni Mteknolojia wa Dawa.