Waumini 11 kati ya 25 waliotekwa nyara siku ya Jumapili baada ya kanisa lao kushambuliwa kaskazini-magharibi mwa Nigeria wameachiliwa huru na watekaji nyara, kiongozi wa kidini aliambia AFP siku ya Jumatano.
Siku ya Jumapili, watu wenye silaha walivamia Kanisa la Bege Baptist katika eneo la Chikun katika Jimbo la Kaduna, na kuwateka nyara watu 40 awali,watu kumi na watano baadaye walifanikiwa kutoroka, wakiwaacha watu 25 mikononi mwa wateka nyara.
“Leo kuna watu 14 bado wanazuiliwa na watekaji nyara, huku waliwaachilia 11,” alisema Mchungaji Joseph Hayab, mkuu wa Chama cha Kikristo cha Nigeria katika Jimbo la Kaduna.
“Waliwatelekeza (msituni) au kuwaachilia wale walioona ni vigumu kuwasimamia kwa sababu ya matatizo ya kiafya, uchovu, au umri wao,” alisema.
“Sio idadi ya mateka inayohesabiwa kwao, kwa sababu hata mmoja atawaruhusu kupata fidia badala yake”, alisema kiongozi huyo wa kidini.
Shambulio hili kubwa ni la hivi punde zaidi katika mfululizo nchini Nigeria ambapo ukosefu wa usalama utakuwa mojawapo ya changamoto kuu kwa Rais mpya Bola Tinubu ambaye anatazamiwa kuchukua madaraka mwishoni mwa mwezi.
Utekaji nyara umekithiri kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria. Mateka hao wanazuiliwa katika kambi zilizofichwa kwenye misitu mikubwa wakisubiri malipo ya fidia, shughuli ambayo imekuwa yenye faida kubwa. Utekaji nyara unaweza pia kuwa suala kati ya jamii zinazopingana.
Mwezi uliopita, watu 33 waliuawa na watu wenye silaha katika kijiji kimoja katika jimbo la Kaduna katika shambulio huku kukiwa na mzozo kati ya jamii za wafugaji na wakulima zinazopigania maji na malisho.
chanzo ;AFnews