Wavuvi 9 wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Victoria Mkoani Kagera wameokolewa baada ya kutelekezwa Ziwani kwa siku 15.
Wavuvi hao ambao walitelekezwa tangu tarehe 8 October mwaka huu, kati yao nane wamepokelewa leo na Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jeneral Charles Mbuge katika Bandari ya Bukoba baada ya kuokolewa wakiwa washaingia upande wa Uganda.
Baada ya mapokezi hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera amekiri kupokea taarifa zao tangu walipotelekezwa na kunyang’anywa baadhi ya vifaa vyao ikiwemo mitumbwi na kuachiwa mtumbwi mmoja huku ukiondolewa baadhi ya vifaa ili usifanye kazi huku Afisa Uvuvi Mfawidhi wa Kikosi cha Doria Mkoa wa Kagera Yohana Milunde akituhumiwa kuwafanyia kitendo hicho.
Meja Jeneral Mbuge amesema kuwa tayari mtu mmoja kati yao alichukuliwa na ndugu zake na kuongeza kuwa Afisa wa Doria anayetuhumiwa tayari yupo mikononi mwa TAKUKURU na kuahidi kuwa wataendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa atakayekutwa na hatia.
MO DEWJI AKASIRIKA “HAIKUBALIKI, WALIOSABABISHA WACHUKULIWE HATUA”