Wawekezaji 71 kutoka mataifa mbalimbali duniani wameonyesha nia na kusaini mikataba ya awali ya kwenda kuwekeza katika eneo la kongani ya viwanda lililo andaliwa kwa uwezeshaji kwa ushiriano wa nchi ya Tanzania na China SINOTAN lililopo Kwala Kibaha mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa na Mhandisi wa mradi Eng. Alexander Nchaholuli wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya uendelezaji wa eneo la kongani ya viwanda huko Kwala Kibaha mkoani Pwani kwa Washiriki 56 wa Mafunzo ya Uongozi kwa Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini kutoka Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani walipofika kujionea maendeleo ya ujenzi wa Bandari kavu na kongani hiyo ya viwanda.
Alisema wawekezaji hao ni sehemu ya wawekezaji wa viwanda zaidi ya 200 vinavyotakiwa kuwekezwa katika eneo la kongani ya Viwanda ya Kibaha ambapo ajira zaidi ya laki moja zinatarajiwa kuzalishwa katika eneo hilo.
Eng. Alexander alisema wanaendeleza eneo hilo kwa awamu ambapo kwasasa wapo kwenye mazungumzo DAWASA, uwekaji wa miundo mbinu ya huduma za maji, Tanesco na ili kuweka umeme pia gasi asilia itahitajika kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa na taasisi hizo.
“Umeme utahitajika mwingi zaidi ya megawatt 250 kwa siku, maji Lita zaidi ya millioni 40 kwa siku ndio maana tunatengeneza hii kongani kwa awamu ambapo awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika mwezi Octoba mwaka huu kwasababu kuna vitu vilihitaji marekebisho”
Alisema eneo hilo la kongani ya viwanda pia wanatarajia kuingiza reli ambayo itasaidia kuingiza malighafi nzito na kubwa kutoka bandarini hivyo eneo hilo litawahi kuchangamka kutokana na uwekezaji mkubwa unaotarajia kufanyika katika eneo hilo la Kwala;
”Kwasababu limezungukwa na eneo la bandari kavu na standi ya reli ya mwendo kasi ya Kwala, kuna viwanja vya makazi na uwekezaji vya Halmashauri kwa upande wa kulia kwahiyo tunaamini eneo hili litakuwa la mwanzo kabisa kuchangamka” alisema Eng. Alexander.
Mshiriki kutoka Katibu wa Taasisi ya Mwalimu Julias Nyerere mkoa wa Pwani Omari Punzi amepongeza na ameshukuru kuona jitihada kubwa serikali inazofanya kuongezea uwezo bandari ya Dar es salaam ambapo sehemu kubwa ya makontena yatawekwa katika eneo hilo la Kwala kwani makontena 3200 kwa siku yatahudumiwa.
Alisema uwekezaji unaofanywa ni mkubwa unahitaji umakini mkubwa kwa maslahi ya taifa hivyo iwapo utaboreshwa vizuri taifa litapata manufaa makubwa ya ongezeko kubwa la mapato kutoka ndani na nje ya nchi wanaotumia bandari yetu ya Dar es salaam.
Aidha Punzi amewataka watanzania kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan ili akamilishe uwekezaji huo kilichopkusudiwa kitimie kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.
Mshiriki kutoka NMB makao makuu William Makoresho alisema eneo lililotengwa kwa uwekezaji wa bandari kavu Kwala ni kubwa kimkakati kwani kuna hekali zaidi ya 2500 za uwekezaji ambapo amewataka watu wa kada mbali mbali kushirikishwa ilikuwa na uchumi shirikishi sambamba makundi yote ya watu kutambua wajibu wao katika kukamilisha malengo taifa iliyojiwekea.
‘