Wazazi na walezi katika Shule ya Sekondari Dareda iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoa Manyara wametakiwa kuacha tabia ya kuwashitaki walimu pindi wanapo waadhabu wanafunzi kwalengo la kuwaonya ili wafanye vyema kitaaluma
Akizungumza katika mahafali 14 ya kidato cha sita Mdau wa elimu Shau Erro Mkurungezi wa shirika la Karimu foundation Tanzania amesema katika Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wazazi kuwashitaki walimu kuhusu adhabu wanazopewa watoto wao jambo linalokati linalo nyima walimu fursa ya kuwajenga watoto kitaaluma.
Aidha akijibu changamoto zilizowasilishwa katika risala ya mkuu wa Shule ya Dareda Sekondari Bw. Shau ameahidi kutoa Photocopy Machine yenye thamani ya shilingi mil.9 pamoja na kuwazawadia walimu shilingi Mil.1 na kuwahidi walimu kama endapo watafaulisha kwa kiwango Cha Division one katika mitihani ijayo atawapatia kiasi kingine kama sehemu ya kuwapa hamasa.
Aisha Mshana Mwanafunzi wa kidato Cha Sita Dareda secondary amesema Shule inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana na Umeme wa uhakika nakuiomba uongozi wa Shule kutafuta jenereta yenye uwezo