Baadhi ya wazazi huko Gaza wanaripotiwa kuandika majina ya watoto wao kwenye miili yao kwa kuhofia hawatatambuliwa iwapo watauawa.
Dk Abdul Rahman Al Masri, anayeongoza idara ya dharura katika Hospitali ya Al Aqsa Martyrs, aliiambia CNN kuwa ameona visa vya majina yakiandikwa “miguu na tumbo”.
Alisema inaonyesha wazazi wanahisi “wanalengwa wakati wowote na wanaweza kujeruhiwa au kuuawa”.
Msimamizi mwingine wa hospitali, ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliliita “jambo jipya ambalo limeanzia Gaza”.
“Watoto wengi wamepotea, wengi hufika hapa wakiwa wamevunjwa fuvu la kichwa … na haiwezekani kuwatambua, ni kupitia maandishi hayo tu ndipo wanatambulika.”