Wakazi wa Ukonga, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam wametakiwa kupeleka watoto wao shuleni Gisela kwa elimubora.
Mkuu wa Shule ya Msingi Gisela ambayo ni ya Mchepuo waKiingereza, Malimi Kwilasa anasema kuwa shule hiyo imekuwaikifaulisha kila mwaka kwa wastani mzuri wa A na hivyokuifanya kuwa moja ya shule bora Wilaya ya Ilala.
Pia shule hiyo ina shule ya awali au chekechea.
Anasema matokeo ya mwaka jana darasa la saba shule ilikuwana watahiniwa 92 kati yao waliofaulu kwa daraja la A ni 85 wakati daraja B ni saba tu.
“Hivyo kwa mantiki hiyo utaona namna shule yetuinayofaulisha, wazazi wawalete watoto wao shuleni hapa” anasema
Anasema wakazi wa tarafa ya Ukonga kata ya Kipunguni wanafursa ya kupeleka watoto shuleni hapo ili wapate elimu bora, shule iko Mtaa wa Amani , barabara ya Bombambili.
Mwalimu Kwilasa anasema kuwa mazingira ya kufundishia nibora na shule ina usafiri kwa wanafunzi wa maeneo mbalimbaliya Ukonga na hata nje ya Ukonga.