Leo April 18, 2018 stori ninayokusogezea ni kuwahusu Wazazi wenye dini ya Kiislam nchini Ufaransa wamepelekwa mahakamani baada ya kumpa mtoto wao jina la ‘Jihad’ na kutaka kulisajili.
Serikali nchini Ufaransa baada ya kupata taarifa hiyo waliamua kuwafikisha kwa waendesha mashtaka, ambao sasa hivi wanaendesha kesi hiyo kupingana nalo wakiamini kuwa jina hilo lina muunganiko na ugaidi.
Wazazi hao walijaribu kujitetea kwa kuwaeleza waendesha mashtaka kwamba jina hilo halina maana ya vita vitakatifu kama ambavyo wengi wanafahamu, bali ni nguvu na kuweza kujipigania.
Hata hivyo maafisa wa serikali wa Ufaransa wamesema wamewataka wazazi hao kubadili jina la mtoto huyo ili kumlinda na madhara yake baadaye.
MABISHANO MAHAKAMANI MBOWE NA POLISI (April 17 2018)