Rapper AKA aliripotiwa kufariki jana usiku baada ya kupigwa risasi akiwa Jijini Durban alikokuwa amekwenda kikazi.
“Kwa masikitiko makubwa tunathibitisha kifo cha Mpendwa Mtoto wetu ambaye amefariki kifo cha kusikitisha jioni ya Feb 10,2023, tunasubiri taarifa zaidi kutoka Polisi wa Durban”
“Kwetu Kierman alikuwa Mtoto wetu, Kaka, Mjukuu, Binamu na Rafiki na zaidi Baba wa Mtoto wake Mpendwa wa kike Kairo, kwa Watu wengine wengi alikuwa AKA, SUPAMEGA, BHOVA na majina mengine mengine ambayo Mashabiki zake walimuita”
“Mtoto wetu alipendwa na alirudisha upendo kwa waliompenda, kwenye wakati huu mgumu tunawaomba huruma yenu, mtupe muda na nafasi ya kukutana kama Familia na kuamua taratibu zinaofuata katika siku zijazo, asanteni kwa upendo na ushirikiano wenu tumeupokea na tunaomba muendelee kutuweka kwenye maombi”