Ni Mei 14, 2024 ambapo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega aliwasilisha Bungeni Dodoma Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka 2024/25.
‘Mheshimiwa Naibu Spika katika Mwaka 2023/24 Wizara ilianza kutekeleza mpango wa mabadiliko katika sekta ya mifugo ili kuchangia ipasavyo katika ukuaji wa Uchumi na pato la Taifa na kupunguza Umasikini’Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
‘Unaweza kuona Tanzania imefika kwa mara ya kwanza kutengeneza maziwa ya Unga na kiwanda cha kizalendo cha ASAS ambacho leo nimekuja hapa kuwaonesha Waheshimiwa Wabunge namna ya kazi kubwa na uzuri inayofanywa, haya ni mafanikio Makubwa sans’—Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka 2024/25
‘Mheshimiwa Naibu Spika Wizara imekamilisha imekamilisha mapitio Sera ya Taifa ya Mifugo ya Mwaka 2006 ambapo rasimu ya kwanza iliyoboreshwa ipo katika Hatua za Maamuzi ya kiserikali’-Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
‘Aidha Wizara imekamilika Nyaraka za kuunganisha bodi za Nyama na Bodi za Maziwa na kupendekezwa kwa kuundwa kwa chombo maalum kitakachosimamia uendelezaji wa Mazao na Miundombinu ya Mifugo ambapo zipo kwenye hatua za mapitio katika ngazi za Kiserikali’-Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
‘Mheshimiwa Naibu Spika katika mwaka wa 2023/24 bodi ya Maziwa imesajili jumla ya wadau 411 wa Maziwa, idadi hii ni sawa na asilimia 103 ya wadau 400 walikuwa wamelengwa’-Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
‘Pia Bodi imefanya ukaguzi kwa wafanyabiashara 868 kati ya Wafanyabiashara 1200 walikuwa wamelengwa sawa na 72.3% na hatua stahiki zilichukuliwa kwa wale waliokiuka Sheria’-Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
‘Aidha Serikali imeendelea kuweka Mazingira wezeshi kwa Sekta binafsi iliyopelekea kuanza uzalishaji wa Maziwa ya Unga hapa nchini itakayopelekea kupunguza uagizaji wa Maziwa kutoka nje ya nchi yetu’- Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega