Serikali ya Tanzania inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji katika kusaidia juhudi za uzalishaji na upatikanaji ajira kutokana na viwanda na uwekezaji nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji akiwa Kwala wilayani kibaha akiangalia maendeleo ya uwekezaji unaoendelea Kongani ya viwanda (SINO TAN] ambao mpaka sasa umekamilisha viwanda 2 nje ya zaidi ya viwanda 250 vya kuchakata malighafi na kutengeneza bidhaa ikiiwemo mavazi ndani ya mwaka huu 2023 na kuongezeka kwa uwekezaji na nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania zaidi ya laki 2.
’Nimetmbelea viwanda vimili kati ya 250 na kimoja wapo ni cha nguo [vijora] na taarifa njema nimeambiwa bidhaa zinazotengenezwa zinatumika ndani ya Tanzania na vinasambazwa Dubai pamoja na Zambia nimefurahishwa sana kwahivyo ni wazi taifa letu limeanza kupata fedha za kigeni kutokana na uwekezaji unaoendelea’
‘Leo nimekutana na wawekezaji wa Hunan Pia wao wanatazama namna ya kuwekeza hapa na nimpögeze rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutufungulia Milango ya wawekezaji nchini’
‘Lakini ajira zimetengezezwa kwa ukubwa kwani asilimia 90 ya mabinti waliopata ajira mahali hapa wanatoka hapa hapa kwala hivyo naridhishwa na kasi ya utekelezaji wa yale niliyoagiza mwezi wa 8 na tutegemee ajira zaidi hapa SINO TAN kibaha na changamoto ya kutopata feda za kigeni litatatuliwa na uwekezaji huu hapa na kila kijana uchumi wake utabadilika’