Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amesema TAMISEMI kwa inatoa fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne, mwaka 2021 kubadili machaguo yao ili kutoa mwanya kwa Mwanafunzi kusoma tahasusi (Combination) au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalamu fulani katika maisha yake ya baadaye kwa namna ambayo anatamani yeye mwenyewe au kwa kushauriwa na Wazazi/Walezi wake na kadiri ya ufaulu wake .
“Hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya Wanafunzi hawakujaza kwa uhakika combination au kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao, Mzazi una nafasi ya kushiriki katika zoezi hili kwa kushauriana na Mtoto wako katika machaguo yake”
“Tafadhali Mzazi kubaliana na Mtoto katika machaguo yake ili baada ya zoezi la uchaguzi pasiwepo malalamiko yoyote ya kwamba Mtoto amepangiwa machaguo ambayo hakuyachagua”- Waziri Bashungwa
“Zoezi la wanafunzi kubadilisha machaguo yao litafanyika kuanzia tarehe 30/03/2022 hadi tarehe 19/04/2022. Ninasisitiza kuzingatia muda uliotolewa wa kufanya marekebisho ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia shule na vyuo iweze kuendelea vizuri kwa muda uliopangwa”- Waziri Bashungwa