Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka Viongozi wa Vituo vya Umma vya Huduma za Afya kuheshimu fedha zilizotengwa kwa ajili ya kununulia Dawa ili kuondoa kero ya ukosefu wake.
Ameongeza kuwa, yapo maoni mengi kuhusu ukosefu wa Dawa kwenye Vituo vya Afya kutoka kwa Wananchi hivyo Viongozi wanapaswa kuainisha matumizi ya fedha walizopokea au zilizotoka kwenye mapato yao.
Amesema, ni lazima kufanya upekuzi wa matumizi ya fedha za Dawa, pia vifaa na maabara lazima viheshimike na kufika kwa Mgonjwa ili wananchi wajenge imani na Mamlaka katika kuweza kutatua kero zao.
Vilevile, Dkt. Gwajima amezungumzia tiba asili/mbadala akisema zimekuwa zikisaidia kutibu magonjwa hivyo Serikali inalenga kuimarisha kitengo cha Utafiti wa tiba mbadala.