Wakati Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu 31 kwa tuhuma za kujihusisha na na vitendo vya kihalifu maarufu ‘Panya Road’, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amewaonya wazazi wanaozembea kwenye malezi na hivyo kuzalisha watoto wahalifu.
Dk Gwajima ameeleza hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Mbezi Luisi kuelekea Siku ya Familia inayoadhimishwa ifikapo Mei 15 ya kila mwaka.
Amesema wakati Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji watu hao, wizara yake itafanya uchunguzi wake ili kubaini kama kuna wazazi wanahusika kwa namna moja au nyingine na matukio yanayofanywa na watoto wao.