March 17, 2020 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameihaidi Menejimenti ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) ushirikiano katika kukuza tasnia ya horticulture nchini.
Ahadi hiyo imetolewa na Hasunga alipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Taasisi hiyo zilizoko mkoani Arusha.
Akitoa maelezo mafupi kuhusu tasnia hiyo kwa Waziri, Afisa Mkuu Mtendaji wa TAHA Dkt. Jacqueline Mkindi amemweleza Waziri jitihada zilizofanywa na taasisi hiyo katika kukuza tasnia ya horticulture tangu kuanzishwa kwakwe mwaka 2004.
Aidha Dkt. Mkindi amesema kwa miaka yote licha ya jitihada zinazofanywa na TAHA na manufaa zinazoshuhudiwa na wananchi lakini serikali imekuwa na mchango mdogo kwa kutoitambua tasnia hiyo kama sekta rasmi inayoweza kuwezesha upatikanaji wa ajira na kukuza pato la taifa.
Dkt. Mkindi amesema horticulture ndiyo kilimo chenye manufaa kwa sasa duniani kwani mazao yake yanauhitaji mkubwa na soko la uhakika.
Akitolea mfano wa zao la parachichi, Dkt. Mkindi amesema zao hilo linahitajika kwenye masoko yote dunia na hasa parachichi kutoka Tanzania
Amemwomba waziri kupitia wizara ya kilimo kutoa msaada mkubwa hasa katika kusimamia ushindani wa kibiashara kwa kuzingatia kuwa kuna mataifa yanakuja na mbinu chafu ili kudhoofisha biashara hiyo kwa kutambua kuwa Tanzania itanufaika sana.
Vilevile Dkt. Mkindi amemwomba Waziri kusaidia kusukuma uanzishwaji wa mamlaka ya usimamizi wa tasnia ya horticulture ili kuipa nguvu Zaidi katika kuzalisha na kuongeza pato la taifa, kwani haipewi uzito mkubwa kwa sasa kutokana na kukosekana kwa mamlaka husika ya kusimamia tasnia hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa kilimo Japhet Hasunga, amesema hakuwa na uelewa wa kutosha juu ya tasnia hii hivyo kufanya maamuzi yote kuegemea kwenye takwimu na maelezo kutoka kwa watendaji wa wizara
Aidha amesema kwa ufahamu na uelewa alionao juu ya tasnia hiyo atautumia katika kutoa maamuzi yenye tija itakayosukuma mbele kilimo hasa cha horticulture
Hasunga amesema kuhusu ombi la Dkt. Mkindi kuhusu usimamizi wa soko la nje na kudhibiti propaganda potofu, amesema serikali kupitia wizara yake itashughulikia jambo hilo kwa unyeti wake.
Hata hivyo amesema serikali inashughulikia taratibu kadhaa ili kuwezesha makubaliano ya pande zote za nchi ili kuwezesha kufunguka kwa masoko yatakayofanikisha biashara ya mazao ya horticulture nchini.
Akitolea mfano wa soko la Uchina na Arabuni ambayo amesema serikali na makubaliano ya awali(memorandum of understanding) ambayo inahitaji kutimiza baadhi ya masharti machache na maelekezo kadhaa ili kuifanya itumike
Waziri Hassunga ameiomba TAHA kushirikiana na serikali kikamilifu katika kutoa mwongozo na ushauri wa kitaalum kwa kuzingatia kuwa asasi hiyo ndiyo yenye uzoefu na sekta, hivyo kuwezesha sera mpya kutoa dira thabiti kwa ajili ya ustawi wa kilimo hicho nchini.
NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATOA TAHADHARI JUU YA CORONA “GRADUATION WAZAZI HAWATAKUJA”