Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Suleiman Jafo ametoa wiki mbili kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha,kuhakikisha wanaweka mazingira safi katika sehemu ya kuhifadhia taka katika kata ya murieti ili kupunguza magonjwa ambayo yanaweza kusababishwa na takataka hizo .
Jafo ametoa kauli hiyo wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Arusha ambapo ameifanya katika eneo la dampo la murieti Pamoja na eneo la machimbo ya Moramu katika Kijiji cha Engorora kata ya kisongo wilayani Arumeru Mkoani Arusha .
RC MONGELA ATUA ARUSHA “IKIFIKA MAHALI TUTAELEWANA TU, TUTAFIKA MAHALI KUNA CHA KUPOTEZA”