WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Mendeleo ya Makazi Jerry Silaa anatarajiwa kuongoza Kliniki ya Ardhi kwa mkoa wa Tanga itakayofanyika kuanzia Aprili 22 mpaka 28 mwaka huu ikifanyika kwenye maeneo mawili Kijiji cha Miaka 21 Chumbageni Tanga na Korogwe.
Akizungumza na waandishi wa habari,Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Tanga Tumaini Gwakisa alisema zoezi hilo litafanyika kwenye maeneo mawili ambapo litaanzia Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Tanga eneo la Kijiji cha miaka 21 Chumbageni kuanzia Aprili 22 mpaka 25 mwaka huu.
Alisema baada ya kumaliza kwa Tanga wataelekea wilayani Korogwe ambapo litafanyika kuanzia Aprili 26 mpaka 28 mwaka hu na uendeshwaji wa program hiyo utasimaiwa na itaongozwa na Waziri wa Ardhi Jerry Silaa akiwa na wataalamu wa Wizara hiyo.
“Nichukue nafasi hii kwaalika wananchi wote wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kupata huduma mbalimbali za sekta ya ardhi katika maeneo ambayo kliniki hiyo itafanyika kwani kutakuwa na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambapo Waziri atasikiliza kero mbalimbali za Migogoro hiyo”Alisema
Alisema pia kutakuwa na utolewaji wa elimu kuhusu usimamizi wa ardhi pamoja na uwepo wa kituo jumuishi kitakachotoa huduma ya kupokea maoni mbalimbali na utoaji hati miliki ,ukadiriaji wa kodi ya ardhi na ulipaji wa kodi ya ardhi.
Gwakisa aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuhudhuria na kushiriki ambapo Waziri atakuwepo na wataalamu kutoka Wizarani