Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, (Mb), ameongoza ujumbe kutoka Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Baraza la Usafiri na Utalii Duniani (World Travel and Tourism Council )unaoendelea Jijini Kigali, Rwanda.
Hatua hiyo imefuatia kuthibitishwa kwa Tanzania kuwa mwanachama wa WTTC ambapo uanachama huo pamoja na mkutano huo utaleta chachu kwenye kuleta maendeleo kwenye sekta ya utalii haswa kwenye sekta binafsi pamoja na kuitangaza nchi ili kuzidi kuongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza pato la nchi.
Akiongoza Mkutano Mkuu wa WTTC Mhe. Kairuki amefanya mazungumzo na wawekezaji wakubwa duniani, wafanyabishara wenye uwezo mkubwa wa kuleta watalii kwa idadi kubwa, Taasisi zenye uwezo wa kuleta ufanisi kwenye sekta ya utalii, kuwakutanisha wafanyabishara kutoka nchini na wale wa nchi mbalimbali pamoja na kufanya mahojiano (panelist ) na kuongelea mambo mbalimbali ya Utalii, Uwekezaji na fursa zilizopo Tanzania.
ameishukuru jumuiya , wajumbe na wadau wa WTTC kwa kuikubalia Tanzania kuwa Mwanachama na Ushirikiano wao katika kuitangaza na kuimarisha Utalii wa Tanzania na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na nchi hizo ili kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii duniani.
Mkutano huo unaoendelea nchini Rwanda ulianza 31 Oktoba, 2023 na kufunguliwa Tarehe 1 Novemba na Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, Na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan , Makamu wa Raisi wa Burundi Prosper Bazombanza na Mawaziri wa Utalii kutoka Nchi wanachama wa UNWTO zaidi ya members 1200 , Zaidi wa Mawaziri 10 pamoja na Mashirika ya Kimataifa, Taasisi za kifedha na wadau kutoka sekta binafsi.