Leo October 6 Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amezindua Onesho la saba la Kimataifa la Swahili International Tourism Expo (S!TE!) shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akisoma hotuba Waziri Kairuki amesema Serikali itaendelea na jitihada za kufikia lengo la kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuweka mazingira wezeshi ya kufikia lengo hilo amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais kwa kuwa kinara namba moja wa kukuza sekta ya utali nchini.
Aidha, amesema Serikali inatambua waiibu huo na imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha uwepo wa mazingira yatakayopelekea- utalli endelevu (sustainable Tourism).
“Ni kwa sababu hivo Ripoti va Baraza la Utali na Masuala va Safari Duniani (World Travel and Tourism Council, WTTC) ya Mwezi Mei, 2022, imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 Bora Duniani kwa uhimilivu wa maeneo vake kupokea watalii (sustainability). Matunda ya hatua zinazochukuliwa na Serikali yanaonekana wazi. Leo hii pamoja na athari za UVIK019, tunafurahi kwamba, kasi ya kukua kwa sekta ya utalii wetu ni nzuri.”