Ni Desemba 22, 2022 ambapo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wamefika katika hafla ya tukio kujaza maji katika bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji, Mkoani Pwani.
Na Miongoni waliohutubia katika tukio hilo ni Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba…..“Mhe. Rais ulipoingia Machi, 2021 na ndani ya miezi ya 20 ya uongozi wako mradi umefikia 78% kutoka asilimia 37% ulipoukuta mradi huu, hii inaonesha jinsi Mhe. Rais ulivyousukuma kwa kasi, maneno ya kwamba mradi umesimama, unahujumiwa ni ya uongo”- Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
“Mradi huu haujawahi kusimama na kazi zinafanyika kwa saa 24, iwe ni Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu kazi zinaendelea lengo ni kuongeza kasi na umahiri na Kila siku ya Jumanne iwe jua mvua, sisi viongozi wote huwa tunafanya kikao kujadili maendeleo na changamoto za mradi huu(Julius Nyerere) ili tuweze kwenda vizuri”- Waziri wa Nishati January Makamba katika tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji Mkoani Pwani
“Kwa maelekezo na mawazo yako Mhe. Rais ndio kumechangia mradi huu kufika hapa tulipofika leo na mafanikio ambayo tunayafurahia katika mradi huu yanatokana pia na uongozi wako”- Waziri wa Nishati January Makamba katika tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji Mkoani Pwani
“Yamekuwepo matope mengi, na matusi mengi. Sisi hatukukasirika, hatukulalamika, hatukulaumu mtu kwa sababu tulijua hiyo ndiyo sehemu ya uongozi hasa kwenye mradi kama huu. Tulichofanya sisi ni kufanya kazi ili matokeo yawe ndiyo majibu yetu. Leo hii naamini kwamba tuliyoyaona hapa, baasi yatakuwa jibu ya yale mambo mengi ambayo tulitupiwa.”- Waziri wa Nishati January Makamba katika tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji Mkoani Pwani
“Tumejipanga kwa muda mrefu na sio kwa muda mfupi na tunachoomba ni subira. Hizi za kukatikakatika umeme zitaisha. Lakini sisi tunataka ndani ya miaka 50 ijayo ibaki historia kwamba chini ya uongozi wako Mhe Rais, ndipo ulimaliza shida yote ya umeme ya kudumu” Waziri January Makamba.
MRADI wa Bwawa la Nyerere kwa ujumla umeajiri wafanyakazi wapatao 12,275 hadi kufikia mwezi Novemba 2022. Kati ya wafanyakazi hao walioajiriwa watanzania ni 11,164 sawa na asilimia 90.97 na wafanyakazi toka nje ya nchi ni 1,111 sawa na asilimia 9.1.