Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amekagua Ujenzi wa Maendeleo ya awamu ya tatu ya Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ambayo inagharimu Sh.Bilioni 231.
Katika ukaguzi huo, Prof.Mbarawa amesema kuwa awamu ya tatu ya BRT ambayo ni ya Tazara ina Kilomita 23 ambapo inatarajiwa kukamilika mwaka 2024.
“Katika mji wetu wa Dar es Salaam tunajenga barabara za Mwendokasi BRT tunajenga barabara za mzunguko na barabara nyingine zote hizi tunafanya hivyo ili kupunguza msongamano kwenye jiji la Dar es Salaam, maana ni jiji la biashara na msongamano ni mkubwa”- Profesa Mbarawa
“Tumeanza mfumo wa BRT, tumefanya BRT One, tumekuja Two sasa hivi tupo Three, tutaenda Four na Five na juzi tulizungumzia BRT Six”
“Leo hapa tumekuja kuangalia maendeleo ya uje wa BRT namba Tatu ambayo ina urefu wa Kilomita 23.3 pamoja na vituo mbalimbali na ina gharimu takribani Shilingi Bilioni 231 za Kitanzania,“. Profesa Mbarawa.