Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewataka wananchi kuendelea kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa November 27, 2024.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo October 15, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la
Mwanza kwa lengo la kueleza mwenendo wa zoezi linavyokwenda na umuhimu wa kujiandikisha, Mchengerwa amewataka wananchi wenye sifa na wanaokidhi vigezo vya kugombea wajitokeze kuchukua fomu kuanzia October 26, 2024 hadi November 1, 2024 ili waweze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za Mitaa na Vijiji.
Waziri Mchengerwa ameongeza kwa amewataka wasimamizi wa uchaguzi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, kanuni, miongozo pamoja na maelekezo ya usimamizi wa uchaguzi.
Katika hatua nyingine Mchengerwa amewataka Viongozi wa vyama vya Siasa kutoa elimu kwa wanachama wao kuhusu kujiandikisha na umuhimu wa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa.