Ni siku ya ufunguzi wa maonyesho ya Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi STADI ambayo yanaendelea kufanyika katika uwanja wa sheikh amir Abed Jijini Arusha ikiwa not siku ya NNE tokea yaanze na kufunguliwa rasmi
Maonyesho hayo ni fursa kwa vijana kwakujifunza mafunzo ya ufundi STADI kwa vitendo ili kukuza wigo mpana katika upatikanaji wa ajira swala ambala kwa sasa limekuwa changamoto kubwa kwa vijana na wahitimu wa vyuo.
Waziri Elimu sayansi na technologia profesa Adolf MkendaAmbae ni Mgeni rasmi akizindua maonyesho hayo ameeleza kuwa serikali inajitahidi kutengeneza mahusiano mazuri kati yao na wazalishaji wa huduma pamoja na bidhaa ili vijana waweze kupata mafunzo zaidi kwa vitendo katika vyuo vya ufunzi iweze kuwasaidia wanapohitimu kutoa na ujuzi uliyobora.
Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi STADI ni nyenzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya viwanda ili kufanikisha hilo nimuhimu kuzingatia umahili wakutenda kazi na uwepo wa ushirikiano kwa watoa mafunzo na waajiri ili kutokomeza changamoto ya ukosefu wa hajira,Dr Adolf Rutayuga katibu mtendaji baraza la taifa la elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET)
miongoni Mwa vyuo vilivyoshiriki katika maonyesho hayo ni chuo cha Jeshi la Zimamoto Tanzania Naibu kamishina kened komba ambae ni Mkuu wa chuo hicho anasema lengo la kuja katika maonyesho hayo ni kutoa Elimu kwa vitendo kama ilivyo jukumu lao ili kuepukana na ajali za moto na kuwataka wananchi wanapoona dalili ya ajali ya moto watoe taarifa mapema.
Husna Juma Mbunge wa viti maalum Tanga amesema lengo la serikali ni kuhakikisha vijana wote wanapohitimu mafunzo yao kutoka chuo wapate ajira ili waweze kujikimu katika maisha hivyokwa uoande wao wabunge watahakikisha jambo hilo linakamilika.
Maonyesho hayo ni yapili yakiwa chini ya usimamizi wa Baraza la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi STADI NACTIVATE huku yakishirikisha vyuo vya ufundi , huku yakitarajiwa kufungwa may 22 mwaka huu.