Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda amesema Wizara yake inatekeleza haraka maagizo ya Katibu Mkuu wa CCM Dr. Emmanuel Nchimbi aliyoyatoa jana akiwa Usa River Arusha kutaka hadi mwishoni mwa June Wanafunzi wa Vyuo wawe wamelipwa fedha hizo za boom.
Profesa Mkenda ambaye ni Mbunge wa Rombo, amezungumza haya kwenye kikao cha ndani cha Viongozi na Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro mbele ya Katibu Mkuu wa CCM na kusema kuwa Wizara yake imepokea agizo hilo na kwamba watalitekeleza kabla ya mwisho wa mwezi.
“Ndugu Katibu Mkuu jana pale Arusha ulitoa maelekezo kuhusu suala la boom na naomba nitumie nafasi hii kusema kuwa suala hilo tutalifanyia kazi na kabla ya muda uliotoa Wanafunzi wote Nchini watalipwa” – Profesa Mkenda
#MillardAyoUPDATES