Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikuku (kazi Maalum) Captain Mstaafu Mhe. George Mkuchika ameendelea kusisitiza watendaji wa Serikali kusimamia miradi ya maendeleo Ili ikamilike kwa haraka na kuwanufaisha wananchi.
Waziri Mkuchika amesema hayo wakati akizindua mradi wa maji wa Kijiji cha Mangae Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro ya kukagua, kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendendeleo inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo.
Mhe. Mkuchika amesema Serikali inatekekeleza miradi ya maendendeleo Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijami Kwa wananchi ikiwemo maji,elimu,Barabara na afya ambapo amewataka wananchi wa Mangae kuitunza mradi huo wa Maji ili utumike na vizazi vijavyo
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wana Morogoro kwa kuwaletea miradi mbalimbali hususani ya maji.
Pia amesema uwekezaji wa ujenzi wa tenki la maji katika kijiji cha Mangae utaondoa kero ya upatikanaji wa maji ambayo imedumu Kwa kipindi kirefu
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Sospter Lutonja amesema Kwa Sasa Hali ya upatikanaji huduma ya maji katika Mkoa huo kwa vijiji imefikia asilimia 67 huku ifikapo 2025 wanatarajia kufika asilimia 92
Nao baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamefurahia kukamilika Kwa mradi huo na kwamba utarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo ambayo walikuwa wakiifuata kilometa zaidi ya kumi.
Mradi huo umegharimu jumla ya shilingi Milioni 643.7 hadi sasa fedha zilizotumika ni shilingi Milioni 388.8 ambapo mradi huo umefikia asilimia 85% kukamilika ambpo utahudumia wakazi 4049 na kuweza kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji cha Mangae.