Ni nadra kusikia maamuzi kama haya tena kutoka kwa Kiongozi Mkubwa wa nchi kama Waziri Mkuu kutangaza kujishusha zaidi ili kusaidia Watu au taifa lake, hii imetokea Ireland.
Leo Varadkar (41) ambae ni Waziri Mkuu wa sasa wa Ireland aliesomea kazi ya Udaktari kabla ya kuingia kwenye siasa miaka saba iliyopita, ametangaza kuanza kujitolea kutibu Wagonjwa wenye virusi vya corona ambapo atakua akibadilishana kijiti na Madaktari wengine wa zamu Hospitali.
Waziri Mkuu Varadkar amesema kila wiki atakua na siku moja ya kuingia Hospitali kama Daktari na kuhudumia Wagonjwa kwenye Nchi yake ambayo hadi sasa ina Wagonjwa 5,364 na vifo 25 vilivyotokana na corona.
Ireland ni moja ya Nchi zenye idadi ndogo duniani ambapo mpaka mwaka 2016 idadi ya Watu wake ilikua ni milioni sita na laki tano idadi ambayo haipishani sana na Jiji la Dar es salaam ambalo inakadiriwa lina Wakazi zaidi ya milioni 5 kwa sasa.
PAUL MAKONDA: “WACHA NIPATE LAWAMA”
ZARI KUHUSU TANASHA “AJIANDAE KULEA MTOTO WAKE”