Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Songwe, ambapo baadahi ya majengo yamekamilika na kuanza kutoa huduma na mengine yakiendelea kukamilishwa. Hospitali hiyo ambayo ilianza kujengwa 2019, hadi sasa imegharimu bilioni 13.1.
Akizungumza na wananchi, pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki tukio hilo, waziri mkuu amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya afya, huku akisisitiza ujenzi wa hospitali hiyo ni ya kimkakati itahudumia wagonjwa kutoka nchi za jirani Malawi na Zambia.
Ujenzi wa hospitali hiyo umejengwa na kampuni ya MCB, iliyopo chini ya Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, katika tukio hilo mhandisi Victor Ntungamo alimweleza waziri mkuu, majengo yaliyokamilika na kuanza kutumika ni jengo la maabara, OPD pamoja na nyumba ya mtumishi,jengo la mama na mtoto limefikia asilimia 54, EMD na ICU limefikia asilimia 80.
Nae Mkurugenzi wa kampuni ya MCB mhandisi Ivor Ndimbo amesema watahakikisha majengo yaliyobaki yanakamilika kwa wakati na katika ubora, ili wanachi, pamoja na wagonjwa kutoka nchi jirani waendelee kupata huduma bora kama serikali ilivyokusudia.