Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefuta mnada wa nafaka ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Januari 7, 2020 na kuuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kutangaza upya zabuni baada ya kutoridhishwa na taratibu zilifanyika awali.
Waziri Mkuu amesitisha mnada huo wakati akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Ben Asubisye, ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.
“Mahindi yameuzwa kwa bei ya sh. 340 kwa kilo moja ambayo ni chini na bei ya soko kwa sababu bei ya mahindi sokoni kwa sasa ni sh. 800. Zabuni imetangazwa kwa muda mfupi watu wameshindwa kushiriki. Ilifunguliwa saa 8 mchana na imefungwa saa 5 usiku.” Waziri Mkuu