Waziri Mkuu wa Ivory Coast Amadou Coulibaly amefariki baada ya kuugua wakati wa kikao cha baraza la mawaziri.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 alikuwa amechaguliwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, baada ya Alessane Ouattara kusema kuwa hatowania muhula wa tatu.
Gon Coulibaly alikuwa amerudi kutoka Ufaransa ambapo alikuwa amepokea matibabu ya moyo kwa miezi miwili.
Rais Ouattara amesema kuwa taifa linaomboleza, amesema kwamba bwana Gon Coulibaly alianza kuhisi vibaya wakati wa kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri na akapelekwa hospitali ambapo alifariki baadaye.
Kifo chake kitasababisha hali ya sintofahamu kuhusu uchaguzi huo.