Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Uchukuzi ihakikishe kuwa kila palipo na makutano ya reli na barabara kote Nchini Tanzania pawekwe taa za kiashirio au kifungio cha automatiki cha kuzuia na kuruhusu magari ili kunusuru maisha ya Watanzania.
Waziri Mkuu Majaliwa amenukuliwa yafuatayo akizungumza Jijini Dodoma ———> “Kutokana na kuwepo matukio ya ajali za mara kwa mara zinazohusisha treni na vyombo vingine vya moto, TARURA na TANROADS washirikiane na Shirika la Reli nchini kuhakikisha maeneo yote yenye makutano yanaimarishwa kwa kuwekwa mifumo au alama zenye tahadhari ya kutosha kuweza kudhibiti matukio ya namna hiyo”.