Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa walivyopokewa baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Pulkovo, St. Petersburg, Urusi Julai 25, 2023 ambako Waziri Mkuu atamuwakilisha Rais Dkt. Samia kwenye mkutano wa pili wa kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi.
Mkutano huo unaotarajiwa kuanza Julai 27 – 30, 2023, utafanyika jijini St. Petersburg, Urusi ambapo umelenga kuimarisha na kuhamasisha ushirikiano baina ya mataifa ya Afrika na nchi hiyo.
Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Comoro, Azali Assoumani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) wanatarajiwa kuendesha mkutano huo kwa pamoja (Co-Chairing).
Akiwa huko, Waziri Mkuu atashiriki mkutano huo ambao unatarajiwa kukutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Umoja wa Afrika, Urusi, Mawaziri, Mashirika ya Kikanda, Taasisi na Mashirika ya kiserikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Urusi.