Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekua ikifanya utafiti wa viashiria na matokeo ya UKIMWI kila baada ya miaka mitano ambapo mara ya mwisho utafiti ulifanyika mwaka 2016/2017 ambapo data zake ndio zinatumika hadi sasa
Baada ya kufanyika kwa utafiti huo mara hii Serikali imefanya utafiti Tena kwa kuanzia mwaka 2022/2023 ambapo Uzinduzi wa matokeo muhimu Yanatarajiwa kutolewa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa tarehe 1 Disemba siku ya ukimwi duniani.
Jocelyin Rwehumbiza ni mtakwimu mwandamizi ofisi ya taifa ya Takwimu ambapo amesema Utafiti wa viashiria na matokeo ya virusi vya ukumwi nchini Tanzania ni utafiti ambao ulifanyika nchi nzima katika ngazi ya kaya ili kujua hali ya ushamiri wa VVU na UKIMWI na pia idadi ya Maambukizi mapya na ambao wapo katika matibabu ya VVU.
Amesema utafiti huo umefanywa kwa kuzingatia vigezo vyote kwa kuwaomba wakuu wa kaya na hiyari ya upimaji kwa wanafamilia kwa kupima Maambukizi ya VVU na homa ya Ini na wahusika wakipewa majibu yao na kuoatiwa ushauri
Kwa upande wake Salim Nyaga ni mtaalam wa maabara ya Taifa ya afya ya Jamii amesema upimaji wa afya kwa wananchi mbalimbali ulikua ulifikishwa katika maambara hiyo na maabara zingine ili kupata tafiti zenye uhakika
DR George Mgomela ni mkurugenzi wa miradi kutoka CDC Tanzania anasema lengo la shirika hilo kufadhili zoezi hilo ni kuwawezesha wataalam kufanya kazi kwa makaini na utulivu ili kukamilisha utafiti wenye tija
Utafiti huo wa viashiria vya matokeo ya UKIMWI umefadhiliwa na serikali ya Marekani chini ya mfuko wa Rais wa dharura wa kupambana na UKIMWI (PEPFAR)na msaada wa kiufundi unaotolewa na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Marekani (CDC)na ICAP iliyo kwenye chuo kikuu cha Columbia,Marekani pamoja na TACAIDS ,siku ya UKIMWI Duniani inaadhimishwa Disemba mosi kila mwaka na kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro huku Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akitarajiwa kuwa Mgenis Rasmi.