Waziri Mkuu wa zamani wa Mali, Boubeye Maiga, anashikiliwa na polisi akituhumiwa kwa rushwa katika mchakato wa ununuzi wa ndege ya rais wa wakati huo, Ibrahim Boubacar Keita.
Maiga aliyekuwa akishikilia wadhifa huo kuanzia mwaka 2017 hadi 2019, anafikwa na majanga wakati akipewa nafasi kubwa ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
Mwanasheria wake, Kassoum Tapo, amesema kiongozi huyo anashutumiwa kwa ‘upigaji’ wa Dola za Marekani milioni 40 wakati ndege hiyo inanunuliwa mwaka 2014.
Utawala wa Rais Keita uligubikwa na vitendo vya rushwa, hata kufikia hatua ya Shirika la Fedha la Umoja wa Mataifa (IMF) kusistisha misaada yake kwa Mali.