Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, ametangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi CCM, ikiwa ni siku miezi michache tangu atangaze kuachana na CHADEMA na kubainisha kuwa angekuwa mshauri wa chama chochote cha siasa.
Sumaye amefanya uamuzi huo leo Februari 10, 2020 katika Makao Makuu madogo ya Chama hicho Lumumba jijini Dar es salaam.
Sumaye amefikia uamuzi huo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt Bashiru Ally wakati wa vikao vya baraza la udhamini wa chama hicho ambacho kinaendelea Lumumba jijini Dar es salaam.