Taarifa ya Rais Faure Gnassingbe imeeleza kuwa, Komi Selom Klassou ambaye amekuwa Waziri Mkuu tangu Juni 2015 amejiuzulu pamoja na Serikali yake.
Klassou aliwasilisha maombi ya kujiuzulu kwa Rais Gnassingbe ambaye amempongeza yeye na Serikali kwa kazi ambayo wamefanya wakiwa madarakani.
Kumekuwa na matarajio ya mabadiliko katika Serikali baada ya Rais Gnassingbe kushinda Uchaguzi mapema mwaka huu, akiongeza utawala wa familia yake ulioanza tangu 1967, haijafahamika ni lini Waziri Mkuu mpya atateuliwa.