Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amesema atajiuzulu mwezi ujao na hatashiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika Jiji la Napier, Ardern amesema kuwa Februari 7, 2023 itakuwa siku yake ya mwisho ofisini.
“Siondoki kwa sababu majukumu yamekuwa magumu. Ingekuwa hivyo labda ningeacha kazi kwa miezi miwili,” amesema
“Naondoka kwa sababu ya kutoa nafasi hiyo kwa wengine, jukumu la kujua wakati wewe ni mtu sahihi wa kuongoza.” amesema Ardern.
Tangazo la Ardern linakuja wakati chama chake cha Labour Party kikikabiliwa na kampeni kali ya uchaguzi mwaka huu.
Miaka miwili iliyopita chama cha Labour kilishinda uchaguzi katika idadi kubwa ya kihistoria, kura za maoni za hivi majuzi zimeiweka nyuma ya wapinzani.