Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson(55) anatarajia kurudi kwenye majukumu yake ya kiofisi jumatatu ya wiki ijayo baada ya kupona corona ambayo ilimfanya apelekwe ICU, Boris anarejea kazini wakati huu ambapo uchumi wa Uingereza unatajwa kuporomoka kisa corona.
Kumekuwa na mashinikizo kote Uingereza Watu wakiilamu Serikali ya Nchi hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti corona ikiwemo kasi ndogo ya upimaji na upungufu wa vifaa vya kujikinga kwa wahudumu wa afya.
Uingereza hadi asubuhi hii April 26,2020 ina vifo vya corona 20,319 na visa 148,377.