Hamdok ametangaza uamuzi huo wa kuachia ngazi kupitia televisheni huku akisema anaachia wadhifa huo ili kuruhusu mtu mwingine kusaidia taifa hilo kuvuka katika kipindi cha mpito cha mabadilishano ya kidemokrasia ya madaraka.
Ametoa mwito wa kufanyika majadiliano ili kufikiwa kwa makubaliano mapya kuhusiana na namna Serikali hiyo mpya itakavyofikiwa.
Jeshi la Sudan lilifanya mapinduzi Oktoba 25 mwaka jana yaliyoipindua Serikali ya Hamdok, lakini baadaye Waziri Mkuu huyo alirejea kuongoza Serikali, mwezi Novemba.
MFANYABIASHARA AMPIGA RISASI MWENZAKE KISA UGOMVI WAKE NA MKEWE