Serikali imesema itawafutia leseni wafanyabiashara wote watakaongeza bei ya mafuta ya kula tofauti na bei halisi inayoendana na ghrama za uagizaji baada ya gharama hizo kupanda kutokana na athari za ugonjwa wa corona uliozikumba nchi ambazo Tanzania inaagiza mafuta.
Waziri wa Viwanda na biashara Geoffrey Mwambe akizungumza jijini Dodoma amesema serikali imeshachukua hatua katika kupunguza baadhi ya gharama za uagizaji wa mafuta ya kula nchini hivyo wafanyabiashara wasichukulie kama ni fursa ya kujiongezea bei.
Waziri Mwambe pia ameagiza baraza la ushindani nchini FCC kufanya ufuatiliaji wa bei za mafuta na upatikanaji wake kwani hakuna uhaba wa mafuta nchini.
“Naomba nitoe onyo kwa mawakala wakubwa, wakiuza bei kubwa kuliko ambayo kiwanda kimetoa na faida kulingana na mwenendo wa soko nitafuta leseni za biashara” Mwambe