Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
“Katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 212,457,625,000 kwa mchanganuo ufuatao kiasi cha Shilingi 30,503,685,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 18,522,155,000 ni za mishahara na shilingi 11,981,530,000 ni za matumizi mengineyo” ——— Waziri Nape
“Wizara imeratibu mikutano 13 ya Msemaji Mkuu wa Serikali, jumla ya vipindi 25 vya TV vinavyohusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo viliandaliwa na kurushwa hewani, tumejenga studio ya muda Dodoma kwa ajili ya kuzalisha vipindi vya Kitaifa na Kimataifa”- Waziri Nape
“TBC imeboresha maudhui yanayorushwa na imefanikiwa kununua haki za kutangaza Kombe la FIFA la Dunia ambapo michezo 28 ilirushwa TBC1 na michezo yote 64 ilirushwa TBC Taifa na TBC Online, uanzishwaji wa taarifa ya habari kwa kiingereza umeenza November mwaka jana na kupanua wigo wa habari za TBC”- Waziri Nape
“Vituo vya Radio vimeongezeka kutoka 210 mwaka jana hadi kufikia 215 April mwaka huu, Vituo vya TV vimeongezeka kutoka 56 mwaka jana na kufikia 65 April mwaka huu, Wizara imetoa leseni mpya 20 za magazeti na 18 za maudhui ya mtandao, Sekta ya Habari na Mawasiliano imekua kwa kasi ya 6.1%, ukuaji huu unathibitishwa na ongezeko la upatikanaji wa matumizi ya huduma za mawasiliano”- Waziri Nape
“Takwimu zinaonesha laini za simu zilizosajiliwa kuongeza kutoka Mil 55 April mwaka jana hadi Mil 62 April mwaka huu sawa na ongezeko la 11.8%, Watumiaji wa internet wameongezeka kutoka Mil 29.9 April mwaka jana hadi Mil 33.1 April mwaka huu “- Waziri Nape