Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye @napennauye leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo moja ya aliyoyasema kwenye hotuba yake ambayo imesifiwa na Naibu Spika kwa kuwa fupi kwa dakika 25 pekee ni ongezeko la Watumiaji wa Internet Nchini.
“Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki katika matumizi ya teknolojia kupitia TCRA ambapo takwimu zinaonesha laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka Mil 55 .7 April mwaka jana hadi Mil 62 m.3 April mwaka huu sawa na ongezeko la 11.8%”
“Watumiaji wa internet wameongezeka kutoka Mil 29.9 April mwaka jana hadi Mil 33.1 April mwaka huu sawa na ongezeko la 10.7%”——— amesema Waziri Nape.