Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof Joyce Ndalichako amewataka washiriki wa mshindano ya kusherehesha sherehe za Mei Mosi kuendeleza utamaduni wa kushiriki michezo mbalimbali katika maeneo yao ya ili kuleta tija katika shughuli wanazozifanya katika ukuaji wa maendeleo.
Mashindano ya kusherehesha sherehe za Mei Mosi yamezinduliwa rasmi hii leo, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof Joyce Ndalichako, ambapo amewataka wafanyakazi hao kujenga utamaduni wa kuendeleza michezo mahala pa kazi na kuacha kusubiria mashindano yanayoratibiwa na serikali
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa akatumia jukwaa hili kutoa pongezi kwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyokuwa mstari wa mbele katika kuhimiza michezo
Mwasa amesema michezo inafaida kubwa kwa wafanyakazi kwani inaongezeka hali ya molali ya kazi hivyo taasisi zingine zinatakiwa kutosita kutoa wafanyakzi kushiriki katika michezo hiyo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano hayo Khamis Mkanachi amesema maadhimisho ya mwakani wamejipanga kushirikisha na wafanyakazi waliojiajiri ikiwemo bodaboda ,mama lishe kwani na kuwatabua kama wafanyakzi wa sekta binafsi
Mashindano haya yamehusisha wafanyakazi kutoka Wizara na taasisi mbalimbali pamoja na mashirika ya umma na binafsi, ambapo licha ya kuwa ni sihemu ya kusherehesha sherehe za Mei Mosi yanalenga kujenga afya za wafanyakazi na kukmarisha umoja mahala pa kazi, Maadhimisho hayo ya Mei Mosi yakibebwa na kaulimbiu Isemayo Miaka miwili ya Mhe. Rais Dokta Samia Suluhu Hassan imeimarisha michezo na kuongeza ufanisi kazini ambapo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoni Morogoro huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kua mgeni rasmi.