Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 Bungeni Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba BASATA kwa sasa imeendelea kutokimbilia kuwafungia Wasanii kama ilivyokuwa awali.
‘BASATA limeendelea kutoa Tuzo za Muziki wa Tanzania (TMA) kwa mara ya pili mfululizo. Tamasha la utoaji wa Tuzo hizi lilifanyika Dar es Salaam katika ukumbi wa Super Dome, Masaki Tarehe 29 Aprili, 2023. Utuoji wa Tuzo ulihusisha utoaji wa Tuzo maalumu zilizotolewa kwa Taasisi Nne (4) ambazo ni: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Clouds Media Group na Sauti za Busara, Zanzibar. Lengo lilikuwa ni kutambua mchango wao wa kukuza tasnia ya muziki Tanzania. Tuzo ya Heshima ilitolewa kwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne (4)’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘BASATA likiwa kama msimamizi wa Sekta ya Sanaa nchini, lilishiriki katika utoaji wa Tuzo za AFRIMMA nchini Marekani ambapo Watanzania 19 walishiriki na watano kati yao kushinda Tuzo hizo. Wasanii walioshinda Tuzo ni pamoja na Diamond Platnumz (Best Live Act), Rayvanny (Best Male East Africa), Zuchu (Best Female East Africa), Mrisho Mpoto (Best Traditional Artist) na Joel Lwaga (Best Gospel). Pamoja na malengo mengine, ushiriki huo ulilenga kujifunza na kupata uzoefu katika maandalizi na uendeshaji wa Tuzo za Sanaa kutoka katika mataifa mengine’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘BASATA limeanza kutumia mfumo wa Kielektroniki wa usajili na kutoa vibali kwa wasanii na wadau wa sanaa, lengo likiwa ni kuongeza makusanyo ya rasilimali fedha na kudhibiti mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali pamoja na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wasanii na wadau wa sanaa nchini. Mfumo huu unafanya kazi sanjari na mifumo mingine ya Serikali. Katika kuhakikisha mfumo huu mpya wa kielektroniki wa usajili na vibali – AMIS unatambulika na kuweza kutumiwa na wasanii, BASATA limeendelea kutoa elimu na kuwajengea uwezo wasanii na wadau wa sanaa kuhusu matumizi ya Mfumo huu unaopatikana kwa kiungo cha HYPERLINK “https://sanaa.go.tz/” https://sanaa.go.tz/’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘BASATA liliendelea na mageuzi ya kiutendaji na kitaasisi ili kuwa mwezeshaji zaidi wa shughuli za sanaa badala ya kudhibiti. Hivyo, BASATA limeshiriki kuratibu kutatua migogoro ya wasanii kuhusu mikataba waliyoingia ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 zaidi ya migogoro mikubwa mitano (5) imetatuliwa’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“Serikali kupitia Bodi ya Filamu iliratibu uendeshaji wa Tamasha la Tuzo za Filamu na kutoa Tuzo kwa wadau waliofanya vizuri katika fani mbalimbali kwenye Tasnia ya Filamu ambapo kilele chake kilikuwa tarehe 17 Desemba, 2022 Jijini Arusha. Kupitia Tamasha hili, jumla ya Tuzo 45 zilitolewa kwa wadau wa filamu. Kati ya hizo, Tuzo 32 zilitolewa kwa washindi kwenye vipengele mbalimbali vilivyoshindaniwa, Tuzo 10 zilitolewa kwa wasanii/wadau wa filamu wakongwe, na Tuzo 3 zilitolewa kwa viongozi wa Serikali akiwemo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua mchango wake katika kuilea na kuikuza Sekta ya Filamu nchini ikiwemo kufanikisha Tuzo hizo’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“Kupitia Programu ya kuwaendeleza wasanii chipukizi ijulikanayo kama The Coming Film Star iliyotolewa na Bodi ya Filamu iliwajengea uwezo wasanii chipukizi 60 katika masuala ya weledi, utawala wa fedha, pamoja na uwajibikaji. Pia, waandaaji wa filamu 16 walitembelewa katika maeneo yao ya kazi na kupata mafunzo kuhusu uboreshaji wa kazi za filamu. Vilevile, Bodi kwa kushirikiana na Chama cha Waigizaji Mkoa wa Morogoro iliandaa mafunzo yaliyotolewa kwa waigizaji 65 mkoani humo kupitia programu yake ya Taylor-made Training na kuwajengea uwezo katika fani ya uigizaji’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Katika kuendelea kuimarisha uwezo wa tasnia ya filamu katika uzalishaji wa filamu Bodi ya filamu imeingia makubaliano na Asasi ya Busan Foundation for International Cooporation (BFIC) ya nchini Korea Kusini yenye lengo la kuanzisha shule ya filamu (Film Academy) nchini itakayotoa mafunzo kwa wasanii na wadau wetu ili kuwawezesha kuandaa filamu zenye ubora na shindani kimataifa. Aidha, jopo la wataalamu watano lilikuja nchini kutoka Korea Kusini kwa lengo la kufanya upembuzi yakinifu na kujua mahitaji halisi ya uanzishwaji wa shule hiyo’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Bodi iliwezesha maandalizi na kufanyika kwa Tuzo za Filamu kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali zijulikanazo kama UNI-AWARDS zilizotolewa tarehe 4 Desemba, 2022 jijini Dar es Salaam, ambapo jumla ya Tuzo 30 zilitolewa kwa wanafunzi hao’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
‘Katika kipindi hiki Bodi imeweza kutoa leseni za uendeshaji wa shughuli za biashara za filamu na michezo ya kuigiza 180, ambayo ni sawa na asilimia 300 ya lengo la kutoa leseni 60 katika kipindi hicho. Leseni hizo zilitolewa ikiwa ni hatua za urasimishaji wa shughuli na biashara ya filamu nchini. Aidha, Vitambulisho 271 ambayo ni sawa na asilimia 22.6 ya lengo la vitambulisho 1,200 vilitolewa kwa wadau wanaojihusisha na shughuli za Filamu na Michezo ya Kuigiza’ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“Katika kipindi hiki pekee jumla ya miswada na maombi 286 ya vibali vya kutayarisha filamu yamepokelewa na kuchambuliwa, ambapo kati yake, maombi 69 yalikuwa ya watayarishaji kutoka nje ya nchi, na maombi 217 ni ya watayarishaji kutoka ndani ya nchi (Watanzania). Aidha, jumla ya filamu 1,109 zilihakikiwa na kupangiwa madaraja, sawa na asilimia 73.9 ya lengo la filamu 1,500 kwa mwaka mzima. Kati ya filamu hizo, filamu za ndani ya nchi zilikuwa 1,097 na za nje ya nchi zilikuwa 12′ – Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“Serikali kupitia BASATA imeendelea kukuza ubunifu na utengenezaji wa sanaa bora kwa lengo la kuwawezesha Wasanii kuwa Wabunifu na kubuni kazi za sanaa zilizo bora, BASATA liliendelea na mageuzi ya kiutendaji na kitaasisi ili kuwa mwezeshaji zaidi wa shughuli za sanaa badala ya kudhibiti”– Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“Hivyo, BASATA limeshiriki kuratibu kutatua migogoro ya wasanii kuhusu mikataba waliyoingia ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 zaidi ya migogoro mikubwa mitano imetatuliwa, BASATA pi alimekuwa likiwaita Wasanii sio tu pale kwenye upungufu bali hata pale wanapofanya vizuri na kuwapongeza”- Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“Sambamba na hatua hii, BASATA limeendelea kutokimbilia kuwafungia Wasanii kama ilivyokuwa awali bali kunapotokea changamoto zilizokithiri za kimaadili, kama alivyoagiza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Tamasha la Usiku wa Msanii Joseph Mbilinyi”- Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani
“BASATA limeendelea kutoa Tuzo za Muziki wa Tanzania (TMA) kwa mara ya pili mfululizo, Tamasha la utoaji wa Tuzo hizi lilifanyika Dar es Salaam April 29, 2023, ukihusisha utoaji wa Tuzo maalumu zilizotolewa kwa Taasisi Nne ambazo ni UDSM, Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Clouds Media Group na Sauti za Busara, Zanzibar”- Pindi Chana, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo #BajetiYaBurudani