Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa ameanza rasmi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya mkoa wa Mbeya katika Kliniki ya Ardhi ya inayoanza leo tarehe 15 hadi 21 Aprili 2024 katika ukumbi wa Mkapa, Sokomatola jijini Mbeya.
Waziri Silaa aliwasili katika ukumbi huo na ameanza kusikiliza migogoro hiyo ya ardhi saa moja kamili asubuhi kwa lengo la kutatua migogoro ya wananchi wa mkoa huo ambayo imekuwa ikisumbua kwa muda mrefu.
Miongoni mwa kesi alizokutana nazo Waziri Silaa, ni bibi Mbaye amealamika kuporwa eneo lao na jiji la Mbeya kwa kupima na kugawia watu viwanja, eno ambalo hapo awali lilikiwa ni kiwanja cha michezo.
Aidha, Waziri Silaa ameahidi kulitembelea eneo hilo siku ya juma tano tarehe 17 Machi 2024 ili kupata ufafanuzi wa kina na kutatua mgogoro huo.