Ni Julai 29, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kweny Mkutano wa Chama ulioandaliwa Kawe Jijini Dar es Salaam huku akiongozana na viongozi mbalimbali wa Chama hicho.
Hapa nimekusogezea Nukuu za Mhe Abdallah Ullega Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
“Nieleze kwa ufupi upotoshwaji unaosemwa kwamba baada ya kuingia mkataba huu, hatutaruhusiwa tena kufanya jambo jingine lolote linalohusiana na bandari katika taifa letu”- Mhe Abdallah Ulega Waziri wa Mifugo na Uvuvi
‘Ibara ya 43 ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi inaelekeza serikali kujenga bandari ya uvuvi. Na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt Rais Samia Suluhu Hassan imeianza kazi hiyo kujenga bandari ya uvuvi pale Kilwa na tayari Sh Bilioni 40 zilishawekwa na kazi inaendelea,” Mhe Abdallah Ulega Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
‘Serikali ya Rais Samia ina mpango wa kuongeza wigo kujenga bandari nyingine pale Bagamoyo. Hatua mbalimbali zinaendelea. Na ndio maana inashangaza kuona baadhi ya watu wanasema kwamba tukishaingia kwenye uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam hatutakuwa na ruhusa ya kuendeleza bandari nyingine. Huo ni uongo.” Mhe Abdallah Ulega Waziri wa Mifugo na Uvuvi.