Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itafanya warsha ya siku mbili na wadau wa Uendelezaji Milki Nchini ‘ real Estate’ili kusimamia Sekta ya Milki na Nyumba ili kuboresha manufaa ya kiuchumi yatokanayo sekta hiyo.
Akifafanua zaidi kuhusu maana ya Milki (Real Estate), Kabyemela amebainisha kuwa inaweza kutumika pia kumaanisha biashara ya kununua, kuuza au uwekezaji kwenye ardhi, nyumba na majengo kwa matumizi ya biashara.
Mkutano huyo wa Wadau wa Sekta hiyo utakaofanyika tarehe 1 & 2 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Kisenga – Millenium Towers, Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Kauli mbiu ya Mkutano huu ni Ukuaji wa Sekta ya Milki kwa Maendeleo endelevu ya jamii na uchumi.
Wadau mbalimbali wametaliwa kujitokeza kwa wingi ili kubadilishana mawazo na kuchochea ukuwaji wa sekta hiyo.