Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela, Diosdado Cabello, amekanusha madai kwamba Ndege iliyokamatwa nchini Guinea-Bissau ikiwa na kilo 2.6 za Cocaine ilitoka Venezuela.
Amesema hayo alipomkuwa akizungumza kwenye tukio la Serikali Jumatano, Cabello alisema kwa msisitizo, “Ndege hiyo haijawahi kugusa ardhi ya Venezuela.”
Aidha Polisi wa mahakama wa Guinea-Bissau, wakishirikiana na Wakala wa Kupambana na Dawa za Kulevya wa Marekani (DEA) na Kituo cha Uchanganuzi wa Uendeshaji Baharini wa Dawa za Kulevya (MAOC-N) walitekeleza operesheni hiyo mnamo Septemba 7, na kuwatia mbaroni Wafanyakazi watano wa Ndege hiyo, wakiwemo Raia wa Mexico, Colombia, Ecuador, na Brazil.
Licha ya ripoti za awali kudai Ndege hiyo ilitoka Mexico, waziri wa mambo ya ndani wa Venezuela alisisitiza kuwa nchi yake haizalishi Dawa za kulevya, huku akimlenga Marekani kama “mtumiaji mkubwa wa Dawa za kulevya” duniani.
Guinea-Bissau imekuwa njia muhimu kwa usafirishaji wa Dawa za kulevya kimataifa, hususan kutoka Amerika ya Kusini na Asia Kusini Magharibi kwenda Ulaya, na ripoti ya Umoja wa Mataifa imebainisha ongezeko la matumizi ya Afrika Magharibi katika biashara hiyo ya kimataifa ya Dawa za kulevya.