Wakati wa ziara katika Kambi ya Wakimbizi ya Jalazone katika ukingo wa Magharibi, waziri wa mambo ya nje alitangaza msaada wa pauni milioni 10 wa ufadhili kwa shirika la misaada na kazi la umoja wa mataifakuokoa maisha kwa wakimbizi wa Kipalestina..
kifurushi chenye thamani ya pauni milioni 10 kitachangia utoaji wa huduma za UNRWA, ikijumuisha utoaji wa elimu kwa watoto wapatao 543,000 na huduma za afya kwa wakimbizi milioni 1.9 wa Kipalestina.
Waziri wa Mambo ya Nje alionya kuhusu ‘mgogoro wa kibinadamu’ unaowakabili wakimbizi wa Kipalestina na kuitaka jumuiya ya kimataifa kufuata mwongozo wa Uingereza juu ya UNRWA na kuongeza uungaji mkono wao.
Ufadhili huo wa ziada utajibu mzozo unaozidi kuwa mbaya kwa wakimbizi wa Kipalestina.
Kuongezeka kwa mchango wa kila mwaka wa Uingereza kwa UNRWA utasaidia shirika hilo kuendelea kutoa elimu kwa karibu watoto 543,000 kwa mwaka – nusu yao wakiwa wasichana – na kutoa huduma za afya kwa wakimbizi milioni 1.9 wa Kipalestina katika eneo hilo.
Wakimbizi wa Kipalestina milioni 5.9 waliosajiliwa wanasimamiwa na mamlaka ya shirika hilo.