Kufuatia mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia na Azma ya Mhe. Rais ya kumtua mama kuni kichwani, Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TABWA), imeandaa Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia litakalofanyika tarehe 22-24 Junk, ukumbi wa SuperDome Masaki- Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa TABWA Noreen Mawalla amesema Lengo ni kutoa elimu, kupanga mikakati ya utekelezaji.na kujenga mtandao wa Biashara. Walengwa ni Wanawake, Vijana, wauza mkaa, watengeneza na Wauzaji wa majiko ya Nishati Safi,Wamiliki wa Migahawa, shule, hoteli, vyuo,wataalam wa afya na mazingira na wadau wengine wote wanakaribishwa kwa ajili ya kupata elimu na kujenga mtandao wa Kibiashara Kupitia Nishati Safi ya Kupikia.
Ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Wizara ya Nishati nchini Mheshimiwa January Makamba.