Waziri wa Madini Anthony Mavunde amezungumza na waandishi wa habari katika Warsha ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na SGS ili kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii kwa kuwafundisha wanafunzi hao na kuendeleza kizazi hiki ambapo takribani wanafunzi 40 kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM pamoja na chuo cha DIT walihudhuria.
Waziri Mavunde amesema kiu ya serikali ni kuona watanzania wanashiriki rasilimali ambazo wanazitumia. Amesema kwasasa Kuna mabadiliko ya sheria ambayo inawapa nafasi watanzania kuwajengea uimara katika sekta ya madini, nishati na nyinginezo.
Waziri Mavunde amesema kutokana na utafiti ambao umefanyika 16% pekee ndo imefanya sekta ya madini yamesaidia kuongezea pesa ya kigeni zaidi 56% nchini.
SGS wanaendana na mpango wa serikali wa kuendelea kuongeza nguvu katika kuwaongezea uwezo watanzania ili waweze kunufaika.
Serikali kupitia Wizara ya madini imesema imebadilisha sheria kwenye baadhi ya maeneo ambayo inawaruhusu watanzania wengi zaidi kunufaika na sekta ya madini kupitia maudhui ya ndani ili kuwapa fursa ya kujikwamua kiuchumi na kukuza pato la Taifa.
Sekta ya madini ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi ambapo zaidi ya asilimia hamsini na sita ya fedha za kigeni zinatokana na sekta hiyo kutokana na kauli ya Waziri mwenye dhamana ya madini nchini.